1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watatu wauawa na zaidi ya mifugo 200 waibwa Isiolo

20 Februari 2023

Watu watatu wameuawa na zaidi ya mifugo 200 kuibwa katika kaunti Isiolo nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/4Njpu
Äthiopien Addis Abeba Shegole-Schlachtviehmarkt
Picha: Seyoum Getu/DW

Inaaminika kuwa wavamizi hao waliwaua wafugaji wawili baada ya kuiba bunduki kutoka kwa polisi wa akiba waliyemuua baadaye.

Wakaazi wa Isiolo wanasema mashambulizi hayo yanatokana na mpango wa serikali wa kuwanyang'anya watu silaha haramu katika maeneo mengine na wameitaka serikali kukituma kikosi cha jeshi la ulinzi kama ilivyofanyika katika maneo mengi ya nchi ambayo yanakabiliwa na visa vya wizi wa mifugo.

Afisa Mkuu wa polisi eneo hilo, Hassan Barua, na mratibu wa jimbo hilo, George Odiming, wamesema kuwa polisi wameanza uchunguzi wa kurejesha ngamia walioibwa.

Polisi wanaamini kuwa wavamizi hao wametorokea jimbo jirani la Samburu. Inasemekana kuwa watu 10 wameuawa katika eneo la Mulango tangu mwaka huu uanze.