1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasiasa 16 wajitokeza kuwania urais wa Urusi Machi, 2024

20 Desemba 2023

Wanasiasa 16 wamejitokeza kuwania kiti cha urais nchini Urusi katika uchaguzi wa mwaka ujao ambao Rais Vladimir Putin anatazamiwa kushinda kwa urahisi muhula wa tano madarakani.

https://p.dw.com/p/4aPgS
Urusi | Putin kuwani muhula wa tano uchaguzi wa 2024.
Urusi itafanya uchaguzi wake mkuu Machi 2024.Picha: Yevgeny Biyatov/AFP/Getty Images

Shirika la Habari la Urusi, RIA, limemnukuu kiongozi wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo Ella Pamfilova akitoa tangazo hilo hii leo, wiki moja kabla ya siku ya mwisho ya wagombea kujisajili ambayo ni Desemba 27.

Rais Putin tayari alitangaza mapema mwezi huu dhamira ya kuwania muhula wa tano katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Machi 15 mwaka 2024.

Soma pia: Putin kuwania urais 2024

Kwa miaka kadhaa sasa utawala mjini Moscow umekuwa ukifanya ukandamizaji dhidi ya viongozi wa upinzani hususani nyakati za uchaguzi, mwenendo unaomsafishia njia kila wakati Rais Putin kupata ushindi wa kishindo.