1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin kuwania urais 2024

8 Desemba 2023

Rais Vladmir Putin wa Urusi ametangaza kuwa atawania tena kiti cha urais mwaka 2024, hatua inayomruhusu kiongozi huyo wa Kremlin kurefusha utawala wake wa miongo kadhaa hadi miaka ya 2030.

https://p.dw.com/p/4ZwrA
Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Rais Vladimir Putin wa Urusi.Picha: picture alliance/dpa/TASS

Putin, mwenye umri wa miaka 71 ameiongoza Urusi tangu mwanzoni mwa karne hii, huku akishinda urais mara nne na kwa muda mfupi kuwa waziri mkuu katika mfumo ambao hauna upinzani kabisa.

Tangazo la Putin limetolewa katika hafla maalum ya kuwapongeza wanajeshi, ikiwemo wale waliopigana katika operesheni ya kijeshi nchini Ukraine, ambayo Putin aliamuru Februari mwaka uliopita.

Soma zaidi: Putin atia saini sheria inayomuezesha kuongoza hadi 2036

Akizungumza katika hafla hiyo, Putin amesema hatoficha, kwamba amekuwa na mawazo tofauti katika wakati tofauti, lakini huu ni wakati ambapo uamuzi unapaswa kufanywa.

Alikuwa akizungumza na Luteni Kanali Artyom Zhoga, afisa wa kijeshi wa Urusi ambaye muda mfupi kabla ya hapo alimuomba Putin agombee urais.