1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Putin kugombea muhula mwingine uongozini kama mgombea huru

16 Desemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin atagombea tena kiti hicho katika uchaguzi mkuu ujao kama mgombea huru mwenye uungwaji mkono mkubwa lakini sio kupitia tiketi ya chama

https://p.dw.com/p/4aFfV
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa kongamano la kila mwaka la wanahabari mjini Moscow, Desemba 14,2023
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Zemlianichenko/REUTERS

Vyombo hivyo vya habari vimeendelea kuripoti kuwa kundi la wanasiasa zaidi ya 700 na watu kutoka sekta ya michezo na utamaduni walikutana leo mjini Moscow na kuidhinisha kwa kauli moja uteuzi wa Putin kama mgombea huru.

Soma pia:Uchaguzi mkuu wa Urusi kufanyika Machi 17, 2024

Andrei Turchak, afisa mkuu katika chama tawala cha United Russia (UR) amenukuliwa na shirika la habari la RIA akisema kuwa zaidi ya wanachama milioni 3.5 na wafuasi wa chama hicho, watashiriki kikamilifu katika kampeini za uchaguzi na kusema kwamba Putin alikuwa mmoja wa waanzilishi wa chama hicho.

Soma pia:Putin kuwania urais 2024

Wafuasi wa Putin wamesema kuwa kiongozi huyo amerejesha utulivu, hadhi ya kitaifa na mshikamano ambao Urusi ilipoteza wakati wa machafuko ya kuvunjika kwa muungano wa kisovieti huku wakiongeza kuwa vita vyake nchini Ukraine ambavyo Putin amevitaja kuwa ''operesheni maalumu ya kijeshi'' ni vya haki.