1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu wa Urusi kufanyika Machi 17,2024

7 Desemba 2023

Bunge la Urusi limepanga tarehe 17 mwezi Machi mwaka ujao kuwa siku ya uchaguzi wa rais, ambapo rais wa muda mrefu Vladimir Putin anatarajiwa kugombea tena

https://p.dw.com/p/4ZsLV
COP28 Climate Summit Russia Ukraine
Rais wa Urusi, Vladimir Putin Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Katika mkutano ulioonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni, maseneta, waliidhinisha tarehe hiyo kwa kauli moja hatua inayoashiria kuanza kwa kampeni ya urais. Putin, ambaye amekuwa madarakani nchini Urusi akiwa rais au waziri mkuu tangu mwaka 2000, hajatangaza rasmi ikiwa atagombea, lakini anatarajiwa kufanya hivyo. Uchaguzi huo utafanyika miaka miwili baada ya Urusi kuanzisha kile inachokiita operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine iliyoanza mnamo mwezi Februari mwaka 2022 na baadaye kujinyakulia mikoa ya Ukraine ya Lugansk, Donetsk, Kherson na Zaporizhzhia.