1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibada ya Hajj yaanza rasmi Makkah

6 Julai 2022

Ibada ya hajj kwa waumini wa dini ya kiislamu inaanza rasmi hii leo katika mji mtakatifu wa Makkah nchini Saudi Arabia. Maelfu ya waumini wamekusanyika katika mji huo wakitokea nchi mbali mbali duniani

https://p.dw.com/p/4Dk7X
Saudi-Arabien I Pilger in Mekka
Picha: Ashraf Amra/APA/ZUMA/picture alliance

Ibada ya Hajj ni nguzo ya mwisho katika nguzo tano za imani ya kiislamu na ni ibada inayohimizwa kufanywa na kila muumini aliyekuwa katika uwezo wa kiafya na kiuchumi.

Hii leo katika mji mtakatifu wa Makkah maelfu ya waumini wamekusanyika kuanza rasmi ibada hiyo ambayo tangu lilipozuka janga la virusi vya Corona takriban miaka mitatu iliyopita ndiyo inayofanywa na watu wengi baada ya Saudi Arabia mwezi Aprili dkutangaza  kuruhusu jumla ya waumini milioni moja kushiriki.

Mwaka 2020 na 2021 Saudi Arabia ilizuia raia kutoka nchi za kigeni kushiriki ibada hiyo kutokana na mripuko wa janga la Corona lililopiga duniani.

Hii ni ibada ambayo kwa baadhi ya waumini kwao ni ya kihistoria na mmoja wa waumini hao ni Adam Mohammed raia kutoka nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 53,mhandisi wa masuala ya umeme ambaye amegonga vichwa vya habari kwa kipindi cha miezi kadhaa baada ya kuianza safari yake ya kuelekea Makkah kwa miguu mwaka jana.

Soma pia:Waislamu milioni 1 wahudhuria ibaada ya Hajji Mecca

Mohammed ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Iraq,yeye aliamua kutembea zaidi ya kilomita 7,000 kwa miguu akisukuma kigari alichotia vitu vyake vya matumizi kutoka  Uingereza  akipitia nchi tisa kabla ya kuvuka kutoka Jordan na kuingia Saudi Arabia katika mji wa Tabuk kaskazini magharibi.

Iraker Adam Muhammed wanderte in 11 Monaten von Großbritannien nach Mekka
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika ibada MakkaPicha: Ashraf Amra /AA/picture alliance

Hivi sasa Adam Mohammed ni miongoni mwa wanaoshiriki ibada hiyo akizungumza na shirika la habari la AFP amesema alilia sana alipowasili na hakuamini macho yake,safari yake ilimchukua miezi isiyopungua 11 akilazimika kupunmzika sehemu chungunzima.

Ibada hiyo ni nguzo muhimu kwa imani ya kiislamu

Nguzo za Uislamu ni tano ambazo ni shahada yaani kuukiri uislamu kwa kuamini Mungu ni mmoja tu na Mohammad ni mtume wa Mwenyenzimungu.

Swala ni nguzo ya pili ikifuatiwa na zakat, funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na ya mwisho ni nguzo ya Hajj ambapo waislamu wenye uwezo wa afya na kiuchumi wanatakiwa alau mara moja katika uhai wao kuitimiza nguzo hiyo.

Ingawa janga la Corona lilisababisha vizuizi na maelfu ya waumini kutoka nje ya Saudi Arabia waliotaka kushiriki  wamelazimika kuiweka pembeni mipango yao hiyo.

Soma pia:Wazanzibari kupokea chanjo ya Covid-19 kabla Hija?

Kawaida hajj ni moja ya ibada ya dini  inayoshuhudia mkusanyiko mkubwa kabisa duniani ambapo kiasi watu milioni 2.5 walishiriki mnamo mwaka 2019 kabla ya mripuko wa janga hilo la Corona.

Mwaka uliofuatia wageni walizuiwa na idadi ya mahijaji ikapunguzwa hadi kufikia watu 10,000 walioruhusiwa kuhijj makkah.Aicha binti wa miaka 18 ni miongoni mwa wanaofanya hajj ya mwaka huu akitokea nchini Dagestan.

Mekka I Eine Million Pilger zum Hadsch erwartet
Waumini wakiwa katika ibada MakkaPicha: Amr Nabil/AP/picture alliance

"Niko hapa kuhijj na ni fursa kwangu ya kutembelea Jabal Al Nour,ni muhimu sana katika uislam" Alisema na kuongeza kwamba eneo hilo ambalo ndiko ulikoanza uislamu na mtume Mohammad alikuweko kwenye eneo hilo.

Kuwepo kizuizi kwa waumini walioko nje kushiriki ibada hiyo nijambo ambalo limesababisha hali ya kuvunjika moyomiongoni mwa waislamu duniani ambao kimsingi wengi hukusanya fedha kwa miaka ili kutimiza nguzo hiyo.Japokuwa mwaka huu idadi ya wanaoshiriki ni kubwa bado kuna masharti yaliyowekwa.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW