1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mazungumzo ya kurefusha mkataba wa nafaka yakaribia kufikiwa

12 Mei 2023

Uturuki imesema kwamba mazungumzo ya kurefusha mkataba wa kuruhusu usafirishaji nafaka kutoka Ukraine kupitia bahari nyeusi yanakaribia kupata mwafaka

https://p.dw.com/p/4RGJ1
Ukraine | Getreideernte
Picha: Alexey Furman/Getty Images

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar ametowa taarifa akisema makubaliano yanakaribia kufikiwa katika mazungumzo yanayofanyika mjini Istanbul kati ya maafisa wa nchi hiyo,Urusi na Ukraine pamoja na Umoja wa Mataifa. Rais Recep Tayyip Ergodan pia ametowa taarifa kuhusu kinachoendelea. Mkutano huo pia umejikita kutazama pendekezo la Umoja wa Mataifa la kutaka kuanza tena kwa usafirishaji wa Ammonia inayotumika kwenye mbolea, kutoka Urusi  kupitia bomba la Togliatti na Odessa. Urusi imezishutumu nchi za Magharibi kwa kuzuia kinyume cha sheria usafirishaji wa bidhaa hiyo.