1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Uturuki atangaza kurefushwa mkataba wa nafaka

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza kurufeshwa kwa makubaliano ynayoruhusu usuafirishaji wa nafaka za Ukraine kuanza tena baada ya uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4Ot0P
Türkei Ankara | Präsident Recep Tayyip Erdogan gibt neuen Wahltermin im Mai bekannt
Picha: Adem Altan/AFP

Erdogan amesema wamefikia muafaka baada ya mazungumzo kati ya pande mbili, kuhusu makubaliano hayo yaliokuwa yanamalizika muda wake usiku wa manane leo. Hata hivyo hakusema makubaliano hayo yamerefushwa kwa muda gani.

Soma zaidi Ukraine, UN zataka kurefushwa mpango wa kusafirisha nafaka

Ankara ilisema awali kwamba ilitaka urefushwaji wa siku 120, huku Urusi ikipendelea yaongezewe siku 60. Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine Februari 2022, ulisababisha bandari zake kwenye bahari nyeusi kuzuwiliwa na meli za kivita.

Lakini makubaliano yalioratibiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa Julai 2022, na kusainiw ana Kyiv na Moscow, yameruhusu njia salama za usafiirishaji wa nafaka muhimu. Mkataba wa awali uliongezwa muda hadi Machi 18.