1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaendelea kushambulizi eneo la Donetsk

8 Novemba 2023

Watu watatu wamekufa leo baada ya majeshi ya Urusi kushambulia kijiji cha Bagatyr mashariki mwa mkoa wa Donetsk.

https://p.dw.com/p/4YaLc
Kamanda wa Urusi akiwa katika uwanja wa vita Ukraine
Kamanda wa Urusi akiwa katika uwanja wa vita UkrainePicha: Alexander Polegenko/TASS/dpa/picture alliance

 Kijiji hicho kipo umbali wa kilomita 80 kutoka mji wa Avdiivka katika eneo la viwanda ambalo Moscow ililinyakua kinyume cha sheria mwaka jana.

Idara ya huduma za dharura nchini Ukraineimesema shambulio hilo liliharibu nyumba za watu binafsi na kusababisha vifo vya wanaume wawili na mwanamke mmoja.

Mapigano makali yanaripotiwa eneo la mashariki mwa Ukraine, ikiwa ni zaidi ya miezi 20 tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini humo. 

Soma pia:Urusi yafanya mashambulizi ya makombora na droni usiku kucha Ukraine

Hayo yakijiri, Ukraine imetangaza hii leo kuwa imehusika katika mauaji ya mwanasiasa anayeungwa mkono na Urusi Mikhail Filiponenko aliyeuawa katika shambulio la bomulililotegwa kwenye gari yake mashariki mwa Ukraine.

Filiponenko alikuwa mbunge katika Bunge la jimbo la Lugansk. 
 

Baadhi ya Waukraine waamua kutoroka kuliko kupigana na Urusi