1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafanya mashambulizi ya angani usiku kucha Ukraine

6 Agosti 2023

Urusi imefanya mfululizo wa mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya Ukraine, ikitumia makombora ya angani na ndege zisizoruka na rubani zilizotengenezwa Iran

https://p.dw.com/p/4Up3X
Ukaine Krieg l Nach einem Drohnenangriff in Kiew
Picha: Sergei Supinsky/AFP

Jeshi la Angani la Ukraine limesema mfumo wake wa ulinzi wa angani uliharibu makombora 30 kati ya 40, na droni zote 27 aina ya Shahed ambazo Urusi ilirusha usiku wa kuamkia leo. Hakujatolewa taarifa yoyote kutoka kwa Urusi.

Soma pia: Maafisa wa Urusi wameripoti kwamba meli yao ya mafuta imeshambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani

Haijabainika kama kulikuwa na uharibifu wowote kutokana na shambulizi hilo la usiku kucha. Uwanja wa ndege wa kijeshi ni miongoni mwa maeneo yaliyolengwa katika mkoa wa Khmelnytskyi, magharibi mwa Ukraine.

Wakati huo huo, Urusi imeituhumu Ukraine kwa kukishambulia jana Chuo Kikuu kimoja katika mkoa wa mashariki wa Donetsk. Meya wa Urusi wa mkoa huo Alexei Kulemzin amesema vikosi vya Ukraine vilitumia mabomu ya mtawanyiko katika shambulizi hilo lililosababisha moto mkubwa. Tarifa hizo hazijaweza kuthibitishwa na vyanzo huru.