1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Uingereza yatuma wanajeshi wake kulinda amani Kosovo

Angela Mdungu
7 Oktoba 2023

Jumuiya ya Kujihami ya NATO na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza zimesema kuwa wanajeshi wa awali wa kulinda amani wa Uingereza wamepelekwa katika mji mkuu wa Kosovo, Pristina.

https://p.dw.com/p/4XFG5
Wanajeshi wa NATO wakiwa katika oparesheni
Wanajeshi wa NATO wakiwa katika oparesheniPicha: ARMEND NIMANI/AFP/Getty Images

Wanajeshi hao wameongezwa ili kuimarisha ujumbe wa kulinda amani wa NATO nchini humo, KFOR. Hatua hiyo inatokana na mivutano mipya iliyoibuka kati ya Serbia na Kosovo. 

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema wanajeshi wake watakuwa tayari kufanya operesheni za kijeshi na ujumbe wa kulinda amani nchini Kosovo, chini ya amri ya Jumuiya ya NATO.

Soma pia:Kosovo inasema tabia za Serbia zinafanana na za Urusi kabla ya kuivamia Ukraine

Mivutano ya hivi karibuni ilichochewa na shambulio la kundi la makomando wenye silaha wa Serbia dhidi ya maafisa wa polisi wa Kosovo kaskazini mwa nchi hiyo, mwishoni mwa mwezi Septemba.

Katika tukio hilo, washambuliaji watatu wa Serbia na polisi mmoja wa Kosovo waliuwawa.