1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Kosovo yaonya juu ya tabia ya Serbia ikiifananisha na Urusi

2 Oktoba 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kosovo Donika Gervalla-Schwarz, amesema kupelekwa kwa wanajeshi wa Serbia katika mipaka ya Kosovo kunakumbusha tabia ya Urusi kabla ya kuivamia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4X2hz
Kikosi cha kulinda amani cha Jumuiya Kujihami ya NATO kikiwa katika operesheni zake nchini Kosovo, kufuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi kati ya Kosovo na Serbia
Kikosi cha kulinda amani cha Jumuiya Kujihami ya NATO kikiwa katika operesheni zake nchini Kosovo, kufuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi kati ya Kosovo na SerbiaPicha: Erkin Keci/AA/picture alliance

Waziri huyo wa mambo ya kigeni Kosovo Donika Gervalla-Schwarz anatoa matamshi hayo baada ya Marekani kusema siku ya Ijumaa kwamba inafuatilia kwa karibu mkusanyiko wa wanajeshi wa Serbia karibu na mipaka ya Kosovo inayotatiza usalama wa eneo hilo.

Jumuiya ya kujihami NATO nayo imesema inaidhinisha wanajeshi wa ziada wa kulinda amani kwa ajili ya Kossovo.

Wiki iliyopita rais wa Serbia Aleksandar Vucic alisema hakunuia kuamuru wanajeshi wake kuvuka mipaka kuingia kosovo kwa sababu kuutanua mgogoro kutaharibu mpango wake wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.