SiasaKosovo
Uingereza kupeleka walinzi wa amani 200 Kosovo
2 Oktoba 2023Matangazo
Uingereza imetangaza hatua hiyo katika muda huu ambao kuna wasiwasi wa kukusanyika kwa wanajeshi wa Serbia kwenye eneo la mpaka.
Wizara ya Ulinzi ya taifa hilo imesema zaidi ya wanajeshi 200 watakwenda kuungana na wenzao 400 wa Uingereza ambao wapo Kosovo ikiwa kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka.
Kumekuwa na hali ya kuongezeka kwa mvutano ambapo Jumapili iliyopita, takribani wapiganaji 30 wa Serbia walikabiliana na polisi wa Kosovo katika kijiji cha Banjska huko Kaskazini mwa Kosovo.