1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wavamia makazi ya Imran Khan

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Polisi wamevamia makazi ya kiongozi wa upinzani wa Pakistan Imran Khan yaliyo katika mji wa Lahore mapema leo wakati Khan, aliyewahi kuwa waziri mkuu wa taifa hilo alipokuwa njiani kuelekea mahakamani, Islamabad

https://p.dw.com/p/4Ot4q
Pakistan | Imran Khan | ehemaliger Premierminister
Picha: Akhtar Soomro/REUTERS

Wakati wa uvamizi huo wa polisi, wafuasi wa Khan wapatao 65 walikamatwa. Wafuasi hao waliweka kambi nje ya makazi ya waziri mkuu huyo wa zamani  kwa wiki kadhaa ambako Khan alikuwa akikwepa kuwekwa mikononi mwa polisi baada ya mahakama moja mjini Islamabad kuamuru akamatwe.

Alikubali kuhudhuria mahakamani baada ya jaji kukataa mbali ombi lake la kutaka waranti za kukamatwa kwake zitupiliwe mbali licha ya wafuasi wake kupinga asikamatwe.