Mahakama Pakistan yakataa kuakhirisha hati ya kumkamata Khan
16 Machi 2023Wakili wa Khan ameeleza hayo wakati mamia ya wafuasi wake wakiweka mkesha kwenye nyumba ya mwanasiasa huyo katika mji wa Lahore. Wafuasi wake walipambana na polisi walipojaribu kumkamata kabla ya mahakama kuamuru kutulizwa kwa muda zoezi la kumtia mbaroni hapo jana.
Polisi Pakistan imeachana na jaribio lake la kumkamata Khan
Khan aliondolewa madarakani baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye mwaka uliopita na amekuwa akikabiliwa na kesi kadha wa kadha wakati ambapo anaendesha kampeni ya kutaka uchaguzi ufanyike mapema.
Mwanachama mwandamizi wa chama cha Khan amesema mwanasiasa huyo anahitaji kupewa usalama wa uhakika ili kuweza kufika mahakamani.
Pamoja na mambo mengine Khan anatuhumiwa kupokea zawadi na kuziuza alipokuwa madarakani bila ya kutoa taarifa. Hata hivyo amekanusha madai hayo.