1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Pakistan yafunga baadhi ya maeneo ya Islamabad

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Polisi mjini Islamabad wameyafunga baadhi ya maeneo ya mji huo mkuu wa Pakistan leo wakati aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Imran Khan, akifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili.

https://p.dw.com/p/4OsY4
Pakistan Ausschreitungen in Lahore
Picha: Arif Ali/AFP

Wakazi wa karibu na mahakama itakayosikiliza kesi ya Khan wametakiwa kubaki nyumbani na mikusanyiko ya kisiasa imepigwa marufuku.

Mkuu wa polisi wa Islamabad Akbar Nasir amesema wameweka ulinzi mkubwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo ili kuhakikisha kuwa waziri mkuu huyo wa zamani hatishiwi maisha yake.

Soma pia:Mahakama ya Pakistan yazuia Khan kukamatwa

Imran Khan, aliondolewa madarakani baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye mwaka 2022. Mahakama mjini humo ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwezi uliopita. Khan aliepuka kukamatwa  kwa wiki nzima kufuatia vurugu za wafuasi wake.