SiasaPakistan
Mahakama ya Pakistan yazuia Khan kukamatwa
17 Machi 2023Matangazo
Hatua hiyo ya kumakamata Khan mapema wiki hii iligeuka ghasia wakati wafuasi wake walipopambana na vikosi vya usalama. Vyombo vya habari nchini humo vimesema mahakama kuu ya Islamabad imeifuta amri hiyo ili kumruhusu Khan kufika mahakamani kesho kuhusiana na mashitaka kuwa aliuza kinyume cha sheria zawadi za serikali alizopewa na viongozi wa kigeni wakati akiwa waziri mkuu kuanzia mwaka wa 2018 hadi 2022. Khan anakanusha mashitaka hayo. Tume ya uchaguzi ya Pakistan ilimkuta na hatia na kumzuia kushika wadhifa wa kiserikali kwa muhula mmoja wa bunge.