1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Kikosi kipya cha mashambulizi

Admin.WagnerD11 Februari 2016

Katibu Mkuu wa Jumuiya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema hapo jana kikosi hicho kipya kitakuwa cha kimataifa na kitazunguka katika nchi wanachama za Ulaya ya mashariki badala ya kuwekewa kambi mahala pamoja.

https://p.dw.com/p/1HtoG
US- und afghanische Soldaten in Afghanistan
Baadhi ya wanajeshi wa Nato nchiniPicha: Getty Images/AFP/W. Kohsar

Katibu Mkuu wa Jumuiya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema hapo jana kikosi hicho kipya kitakuwa cha kimataifa na kitazunguka katika nchi wanachama za Ulaya ya mashariki badala ya kuwekewa kambi mahala pamoja.

Stolternberg ameweka wazi kwamba kwa NATO shambulio dhidi ya mshirika mmoja litakuwa sawa na shambulio kwa jumuiya nzima. "Hiki kitakuwa ni kikosi cha kimataifa na ifahamike kabisa kwamba shambulio dhidi ya mshirika mmoja ni shambulio dhidi ya washirika wote"

Kadhalika Stonerberg amekariri kwamba jumuiya nzima itajibu mapigo yoyote. Kikosi hicho kitakuwa cha kimataifa,kitazunguka na kitasaidiwa na mpango wa mazoezi na vifaa vitakavyorahisisha uwekaji wa vikosi vyake kwa haraka."

Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya NATO amesema wataalamu wa mipango ya kijeshi wataamua muundo wa kikosi hicho wakati kipindi cha machipuko.

Brüssel Treffen der NATO-Verteidigungsminister
Wadau wakuu wa kikosi wanachama wa NATOPicha: Reuters/Y. Herman

Uturuki na Ugiriki zimekubali kuiomba NATO kutuma kikosi cha kufuatilia wimbi la wakimbizi katika bahari ya Aegean na kupambana na magenge yanayosafirisha watu kwa magendo.

NATO kutathmini hali ya mzozo na wakimbizi

Uturuki na Ugiriki zimeitaka NATO kutathmini hali hiyo kwa kutumia askari wa ulinzi wa mwambao wa taifa pamoja na idara ya ulinzi wa mipaka barani Ulaya Frontex.

Zikiwa mbioni kuzuwiya wakimbizi kumiminika Ugiriki licha ya kuwepo kwa makubaliano kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya kudhibiti wimbi hilo la wakimbizi Ujerumani na Uturuki ziliwashangaza washirika wenzao wiki hii kwa kusema watalizusha suala hilo kwa jumuiya ya kujihami ya NATO.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von Der Leyen amesema Ujerumani iko tayari kushiriki katika kikosi kitakachoongozwa na NATO kufuatilia wakimbizi katika bahari ya Aegean. "Kwa hiyo ni vizuri kwamba Uturuki imeitaka NATO kuimarisha shughuli zake za uchunguzi katika bahari ya Aegean"

Ameongeza kuwa lengo lazima liwe kufanya iwe vigumu au isiwezekane kabisa kufanyika kwa biashara mbaya kabisa ya kusafirisha watu kwa magendo kwa kutumia uhamiaji haramu, na kwamba hilo litajadiliwa katika mkutano huu na Ujerumani iko tayari kushiriki katika shughuli hizo."

Polen NATO Manöver Response Force (NRF)
Bendera za mataifa wanachama wa NATO pamoja na Zana za vitaPicha: Getty Images/AFP/J. Skarzynski

Umoja wa Ulaya yashinikiza Ugiriki kuboresha kambi za wakimbizi

Umoja wa Ulaya umezidi kuishinikiza Ugiriki kuhusiana na suala hilo la mzozo wa wakimbizi barani Ulaya kwa kuitaka iboreshe mazingira ya wakimbizi na kuimarisha usalama wa mipaka yake venginevyo itazuiliwa kuwa mwanachama wa kanda yake ya kusafiri bila ya paspoti.

Umoja wa Ulaya umesema serikali ya Ugiriki inapaswa iwahudumie vizuri zaidi wakimbizi ili kwamba nchi zilizoelemewa na mzigo huo wa wakimbizi ziweze kuwarudisha wahamiaji katika nchi walikowasili kwanza Ugiriki kwa mujibu wa sheria za umoja huo wenye nchi wanachama 28.

Mwandishi ; Mohamed Dahman/AFP

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman