1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Suluhu ya Merkel kwa Uturuki

9 Februari 2016

Katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa wakimbizi unaoikabili Ulaya, Kansela Angela Merkel amechagua kushirikiana na nchi ambayo ina mapungufu makubwa ya kidemokrasia. Hilo ni hatari kwake, anasema Marcel Fürstenau.

https://p.dw.com/p/1Hrr2
Türkei Ankara Treffen zur Flüchtlingskrise Merkel
Picha: Reuters/U. Bektas

Hivi sasa mgogoro wa wakimbizi utakuwa pia suala la jumuiya ya kujihami NATO. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Merkel na waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu hapo jana, jumuiya hiyo itakuwa na jukumu la kuwazuwia wasafirishaji haramu wa watu katika bahari ya Agean. Majadiliano ya kina juuu ya jukumu hilo la NATO yatafanyika katika mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa jumuiya hiyo utakaofanyika jumatano hii mjini Brussels.

Bila kujali iwapo NATO kweli inastahili kuchukuwa jukumu hilo au la, jambo linalokuja akilini ni kwamba Umoja wa Ulaya haukuwa na mkakati wa pamoja kushughulikia mgogoro huo. Na inapozungumziwa Ulaya hapa, inajumlishwa pia Uturuki, kwa kuwa imekuwa mgombea anaetaka kujiunga na umoja huo tangu mwaka 1999. Licha ya hayo Merkel anataka kuipa nchi hadhi ya mshirika wa mwenye upendeleo. Ujerumani inafahamu tangu muda mrefu hatua hiyo inaweza kumaanisha nini. Sasa masharti yanabadilishwa taratibu moja baada ya jengine.

Erdogan ndiyo ameshikilia mpini

Ikiwa chini ya utawala wa mabavu wa rais Recep Tayyip Erdogan ambaye hana mamlaka lakini mwenye ushawishi mkubwa na mwenye kujiamini, Uturuki ndiyo inazidi kuwa na maamuzi ya juu - kisiasa na hata kifedha. Miongoni mwa haya ni pamoja na makubaliano yaliyofikiwa mnamo mwezi Novemba na kuidhnishwa karibuni, kuipatia nchini hiyo kiasi cha euro bilioni tatu kwa ajili ya wakimbizi wa Syria zaidi ya milioni walioko Uturuki. Ni fedha ambazo zinahitajika haraka kwa kuzingatia hali ngumu inayowakabili wakimbizi, lakini ambayo pia umoja huo uliyogawika unaihitaji ili kuweza kujiokoa, na kuzuwia wakimbizi zaidi kuingia katika Umoja wa Ulaya.

Mwandishi wa DW Marcel Fürstenau.
Mwandishi wa DW Marcel Fürstenau.Picha: DW/S. Eichberg

Na kwa kuwa Ujerumani ndiyo inabeba mzingo mkubwa, vivyo hivyo ndivyo imechukukua jukumu la mlipaji mkuu na ndiyo itakayolipa sehemu kubwa zaidi ya kiasi hicho. Iwapo hilo litarejesha matumaini ya kisiasa aliyoyatarajia Merkel au la, ni jambo linaloweza kutiliwa mashaka. Ingawa wakala wa kulinda mipaka ya Ulaya Forntext umeimarishwa tangu muda sasa, njia hatari za mediterania na kupitia mataifa ya Balkan zinaendelea kutumiwa na wahamiaji. Sasa kuita NATO ije kusaidia ni kukiri kwamba Umoja wa Ulaya umeshinda kufanya wenyewe.

Uturuki haistahili kutathminiwa upya

Kwa Merkel lakini kanuni kuu inabakia kuwa matumaini, hivyo anaendelea kutuma hata msaada wa kiunfundi nchini Uturuki. Wataalamu wa majanga kutoka Ujerumani wanapaswa kuwasaidia Wasyria wanaotoroka mashambulizi ya mambomu ya utawala wa Assad na Urusi. Lakini hali hii haitakuwa ya mwisho kuendelea kuitia mbinyo nchi hiyo jirani. Kuna uwezekano mkubwa kwamba Uturuki itahitaji msaada zaidi katika kipindi cha muda usiyo mrefu. Lakini kila malipo yanayofanyika na kila mkutano na Merkel unamaanisha tathmini mpya ya kisiasa ambayo nchi hiyo haijastahili.

Katika upande wa demokrasia Uturuki iko mbali sana, ukizingatia mgogoro unaoendelea kati ya serikali na Wakurdi pamoja na ukandamizaji dhidi ya uhuru wa habari. Licha ya hayo Ujerumani imeyafumbia macho yote na kuamua kupuuza ukosoaji wa mshirika huyo wa NATO. Ni hivi majuzi tu ambapo mikutano ya mashauriano ilifanyika kati ya viongozi wa Ujerumani na Uturuki.

Ni mwelekeo wa muda tu

Wakati siasa ya Uturuki inafurahia jukumu jipya, kiza kinazidi kutanda kwa Kansela Merkel. Ukweli kwamba amejongea kwa nchi kama Uturuki katika wakati wa shida kama huu, inaweza kuwa ahueni ya muda mfupi tu. Lakini hili halitamsaidia katika kipindi cha muda mrefu, kwa sababu katika mgogoro wa wakimbizi Ujerumani iko nafasi ya usoni. Kuna mamia kwa maelfu wataendelea kuja Ujerumani ambao watahitaji kuhudumiwa na kushirikishwa. Katika hili Kansela Merkel anafanya vizuri kweli. Ushirikiano wake na Uturuki unazingatia uhalisia kwa sasa, lakini kwa bahati mbaya pia haumjengei uaminifu.

Mwandishi. Fürstenau Marcel
Tafsiri: Iddi Ssessanga
Mhariri: Grace Patricia Kabogo