Mazungumzo ya nyuklia ya Iran kuanza tena Jumanne
7 Februari 2022Hayo yameelezwa na Umoja wa Ulaya ambao ndio mwenyekiti wa mazungumzo hayo yanayo fanyika mjini Vienna, Austria.
Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa Vienna mnamo 2018 chini ya utawala wa Rais Donald Trump na kisha kurejesha vikwazo vikali kwa Iran.
Rais wa sasa wa Marekani Joe Bidern ameashiria utayari wa kujiunga tena na makubaliano hayo.
Uingereza, Ufaransa, Ujeruman, Urusi na China bado zinaendelea kuwa sehemu ya makubaliano hayo na zimekuwa zikifanya juhudi za kuyaokoa.
Soma pia: Iran yaonyesha makombora yake ya masafa marefu mjini Tehran
Siku ya Ijumaa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisaini azimio la kuilegezea vikwazo Iran kwa shughuli za kiraia za mpango huo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alipongeza hatua hiyo siku ya Jumamosi lakini akaongeza kuwa haitoshi.
Iran yalenga faida za kiuchumi
Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Saeed Khatibzadeh amesema jumatatu kuwa nchi yake inalenga zaidi faida za kiuchumi kutoka kwenye makubaliano hayo.
"Hakujawa na hatua zozote katika muktadha huu, Marekani imeamua kuchukua hatua katika eneo la maslahi yake yenyewe wakati tunafuatilia kwa karibu hatua zozote kuelekea njia sahihi hatua hizo haziwezi kuchukuliwa kwa uzito", alisema Khatibzadeb.
Soma pia:Rais wa Iran Ebrahim Raisi aapa kisasi kwa mauaji ya jenerali Qassem Soleimani
Wanadiplomasia kutoka nchi tatu za Umoja za Ulaya wamesema wakati mazungumzo yaliposimama baada ya mwezi mmoja Januari 28, majadiliano yalikuwa yanafikia hatua ya mwisho na kwamba hilo lilihitaji maamuzi ya kisiasa.
Chanzo: AP, APTN