1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazoezi ya majini kati ya China, Urusi na Iran kuanza Ijumaa

20 Januari 2022

China, Urusi na Iran zitafanya mazoezi ya baharini ya pamoja siku ya Ijumaa . Taarifa hii imetolewa na, afisa wa mahusiano ya umma wa jeshi la Iran Mostafa Tajoldin siku ya Alhamisi 20.01.2022.

https://p.dw.com/p/45qT2
China Kriegsschiff
Picha: picture-alliance/Photoshot

Tajoldin amesema zoezi la ukanda wa usalama wa baharini la 2022 litafanyika katika eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi na ni zoezi la tatu la pamoja la majini kati ya nchi hizo tatu. Tajoldin amesema China, Urusi na Iran zilianza mazoezi ya pamoja ya bahari mnamo mwaka 2019, na zitaendelea nayo katika siku zijazo.

Soma Zaidi: China, Urusi na Iran zafanya luteka ya kijeshi

Afisa huyo wa Iran amesema madhumuni ya zoezi hilo ni kuimarisha ulinzi na usalama na misingi yake katika kanda hiyo pamoja na kupanua kimataifa ushirikiano kati ya mataifa hayo matatu kwa pamoja kusaidia katika amani duniani, usalama wa baharini na kuunda jamii ya baharini kwa maslahi ya pamoja ya baadaye.

Wanajeshi kutoka vikosi vyote vya jeshi la serikali ya Iran na lile la mapinduzi watashiriki katika mazoezi hayo yanayojumuisha masuala kadhaa kama vile kuokoa meli inayoteketea, kuokoa meli iliyotekwa nyara, na kupiga risasi kwenye shabaha za angani usiku.

Russland | Sitzung der russischen Staatsduma | Iranischer Präsident Ebrahim Raisi
Rais Ebrahim Raisi, anayetambulika kwa misimamo mikali alipozungumza mbele ya bunge la Urusi, Duma.Picha: Anton Novoderezhkin/imago images/ITAR-TASS

Tangu aingie madarakani mnamo mwezi Juni mwaka jana, Rais wa Iran mwenye msimamo mkali Ebrahim Raisi amefuata sera ya "kuangazia mashariki" ili kuimarisha uhusiano na Uchina na Urusi. Iran ilijiunga na shirika la ushirikiano wa Shanghai mnamo mwezi Septemba, shirika la kiusalama la Asia ya Kati linaloongozwa na China na Urusi.

Waziri wa mambo ya nje Hossein Amirabdollahian alizuru China wiki iliyopita na rais wa Iran anakutana na mwenzake wa Urusi mjini Moscow Alhamisi.

Wakati huo huo, Urusi imetangaza Alhamisi (20.01.22) kwamba itafanya mazoezi makubwa ya jeshi la majini yatakayohusisha zaidi ya meli 140 za kivita na meli za usaidizi mwezi huu na katika mwezi wa Februari wakati ambapo mvutano umeongezeka kati yake na mataifa ya Magharibi.

Katika taarifa, ziara ya ulinzi imesema kuwa mazoezi hayo yatafanyika katika bahari za Atlantiki, Pasifiki, Arctic, and Mediterenia na yatahusisha zaidi ya meli 140 za vita, meli za usaidizi, zaidi ya ndege 60, vifaa vya kijeshi na takriban wanajeshi elfu 10