1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

Korea Kaskazini: Jopo la ufuatiliaji wa vikwazo ni batili

20 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Korea Kaskazini Choe Son Hui ameikosoa na timu mpya ya kufuatilia vikwazo inayoongozwa na Marekani na kuonya kuwa nchi zinazohusika na timu hiyo zitaadhibiwa vikali.

https://p.dw.com/p/4m01Y
Korea Kaskazini yalipinga jopo jipya la ufuatiliaji wa vikwazo
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Korea News Service/AP/picture alliance

Ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Marekani, Korea Kusini na Japan kutangaza kuunda timu mpya ya kimataifa ya kufuatilia utekelezaji wa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi yake baada ya Urusi na China kuzuia shughuli za ufuatiliaji wa aina hiyo katika Umoja wa Mataifa.

Soma zaidi: Urusi yatumia kura yake ya turufu kupinga muendelezo wa kufuatilia vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa Pyongyang

Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Machi, Urusi ilipiga kura ya turufu kupinga kuundwa upya kwa jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa ambalo kwa miaka 15 iliyopita limekuwa likihusika kufuatilia utekelezaji wa vikwazo vilivyowekwa kwa nia ya kuzuia programu za nyuklia na makombora za Korea Kaskazini. China haikupiga kura katika mchakato huo.