1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China: Tunatekeleza kikamilifu maazimio ya Umoja wa Mataifa

25 Julai 2023

China imesisitiza kutekeleza maazimio ya vikwazo vya UN, baada ya mataifa ya G7, Umoja wa Ulaya kuitaka kuzifukuza meli za mafuta kutoka kwenye bahari yake ambazo zinaonekana kupeleka mafuta Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4ULI0
China | US Außenminister Blinken in China
Picha: Leah Millis/Pool/REUTERS

Barua iliyotumwa kwa mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa, Zhang Jun, iliibua wasiwasi kuhusu kuendelea kuwepo kwa meli nyingi za mafuta zinazotumia bahari ya  China kurahisisha biashara ya bidhaa za mafutazilizowekewa vikwazo kuelekea Korea Kaskazini.

Soma pia:China yatoa wito wa kuanzishwa tena usafirishaji wa nafaka

Barua hiyo iliyoonekana na shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa, ilitiwa saini na wajumbe wa G7 pamoja na wale wa Umoja wa Ulaya, Korea Kusini, Australia na New Zealand.

Kwa kujibu, China imesema kuwa inatekeleza kikamilifu maazimio ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa na inatimiza kikamilifu majukumu yake ya kimataifa.