Urusi yatumia kura ya turufu kuikinga Pyongyang
29 Machi 2024Matangazo
Hatua hii imejiri wiki kadhaa baada ya kundi hilo la wataalamu kusema linachunguza ripoti ya ubadilishanaji wa silaha kati ya Urusi na Korea Kaskazini.
Uamuzi wa Urusi umezua hisia mseto. Marekani kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje Mathew Miller imesema Urusi imetumia Kura ya turufu kwa manufaa yake binafsi na juhudi za kuzuwia kundi hilo kuchunguza maovu yake na Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini ilipeleka makontena 7,000 ya silaha Urusi
Nayo Wizara ya masuala ya kigeni ya Korea Kusini imesema Urusi imefanya uamuzi usiofaa licha ya kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.