1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chamisa kuendelea na siasa Zimbabwe

26 Januari 2024

Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa amesema atasalia kwenye siasa na anatazamia kuunda chama kipya, siku moja baada ya kujiondoa katika muungano wake wa kisiasa kwa kudai uingiliaji kati wa serikali.

https://p.dw.com/p/4bjRc
Zimbabwe Nelson Chamisa
Nelson Chamisa aachana na Muungano wa CCC aliounda kuelekea uchaguzi mkuu wa 2023.Picha: Tsvangirayi Mukwazhi/AP Photo/picture alliance

Chamisa, ambaye mwezi Agosti alishindwa katika uchaguzi alioutaja kama wa udanganyifu, amesema yuko tayari kwa changamoto mpya baada ya kuondoka kwenye chama cha CCC – Citizens Coalitian for Change.

Soma zaidi: Chamisa alitaka bunge liwarudishe wabunge 15 wa chama chake

Katika mahojiano na shirika la habari la AFP mjini Harare, mwanasiasa huyo alisema ameamua kuondoka kutoka kwa muungano aliouunda miaka miwili iliyopita, baada ya kuingiliwa na chama tawala cha ZANU-PF.

Ameongeza kuwa, wanachohitaji kwa sasa ni mbinu na mwanzo mpya bila ya kufichua jina la chama kipya atakachokiunda.

Soma zaidi:Mbunge wa chama cha MDC akamatwa na polisi 
Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 81, alishinda muhula wa pili madarakani kwa kumshinda Chamisa mwenye umri wa 45 katika uchaguzi ambao waangalizi wa kimataifa walisema haukukidhi viwango vya demokrasia.