1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbunge wa chama cha MDC akamatwa na polisi

7 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EFIq

HARARE

Polisi nchini Zimbabwe imemkamata mbunge mmoja wa upinzani hii leo ikiwa siku mbili baada ya mbunge huyo kuachiliwa huru na mahakama ya wilaya kufuatia madai ya kuhusika katika visa vya kuwahonga watu wanao wanyanyasa wafuasi wa rais Mugabe.Msemaji wa chama cha MDC Nelson Chamisa amesema mbunge huyo Eric Matinenga amekamatwa kutoka nyumbani kwake mapema hii leo na watu watatu waliodai kuwa polisi lakini hakuna sababu iliyotolewa juu ya kukamatwa kwake.Aidha ameongeza kusema uchokozi na vitisho dhidi ya upinzani nchini humo haukubaliki na umepindukia mipaka.Tukio hilo limekuja siku moja baada ya polisi hapo jana kumkamata kiongozi wa chama hicho Morgan Changirai kwa mara ya pili katika wiki moja wakati akiendelea na kampeini ya uchaguzi wa duru ya pili dhidi ya rais Robert Mugabe.

Maafisa nchini humo wamemzuia kiongozi wa upinzani Morgan Changirai kuendelea na kampeini zake za uchaguzi wa tarehe 27 mwez huu. Amri ya polisi imekataza mikutano yote ya kisiasa ya chama hicho cha MDC.Wakati huohuo Umoja wa mataifa na Umoja wa Ulaya umeitaka serikali ya rais Mugabe kubatilisha amri yake ya kuyazuia mashirika ya misaada yasiyo ya kiserikali kuendesha shughuli zao nchini humo kabla ya uchaguzi. Aidha Marekani imeishutumu serikali ya Mugabe kwa kutumia chakula kama silaha kabla ya uchaguzi ujao. Balozi wa Marekani mjini Harare amefahamisha kwamba wapiga kura wanaohitaji msaada wa chakula wamekuwa wakitakiwa kusalimisha kadi zao za kupigia kura ambazo zinaonyesha ni chama gani wanachokiunga mkono.Umoja wa mataifa unakadiria kiasi cha watu millioni 2 huenda wakakabiliwa na kitisho kikubwa cha njaa ikiwa mashirika hayo ya misaada yataendelea kuzuiliwa. Zimbabwe imesema mashirika hayo yataruhusiwa kuendelea na shughuli zao ikiwa wataahidi kutoingilia kati masuala ya kisiasa ya nchi hiyo.