1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baadhi ya Wabunge wataka waziri mkuu wa Ugiriki ajiuzulu

2 Novemba 2011

Habari za kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu mkopo wa Ugiriki imepokewa vibaya na baadhi ya Wagiriki. Wabunge katika chama tawala cha kisoshalisti cha Papandreou jana walichukuzwa na tangazo hilo.

https://p.dw.com/p/133Sx
mkutano wa baraza la mawaziri la UgirikiPicha: picture-alliance/dpa

Mbunge mmoja wa Kisoshalisti alisaliti chama chake, mwingine kutaka uitishwe uchaguzi wa mapema na wa tatu kutaka kuundwe serikali ya muda itakayojumuisha vyama vyote kwa ajili ya kuulinda mpango wa Umoja wa Ulaya. Wengine kadhaa walitaka waziri mkuu huyo ajiuzulu. Bunge la Papandreou lenye uwakilishi mkubwa hivi sasa limekalia ncha kali ya kisu likiwa na kiasi ya manaibu 152 katika viti 300 vya ubunge. Tarehe kamili ya kura ya maoni bado haijapangwa lakini mawaziri wanasema inatarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao.