1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty International: Polsi Italia wanawanyanyasa wahamiaji

Sylvia Mwehozi
3 Novemba 2016

Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International linasema polisi wa Italia wanawapiga na kutumia vifaa vya umeme wahamiaji katika mchakato wa kuchukua alama za vidole .

https://p.dw.com/p/2S4iZ
Mittelmeer Mehr als 6000 Bootsflüchtlinge gerettet
Picha: picture alliance/Pacific Press/A. Di Vincenzo

Katika ripoti ya shirika hilo, shinikizo hilo la Umoja wa Ulaya kwa Italia katika kuwashughulikia wakimbizi na wahamiaji limesababisha kufukuzwa kinyume na sheria pamoja na ukatili dhidi ya wakimbizi ambapo katika baadhi ya kesi inaweza kuwa ni mateso.

Mchakato wa kuchukua alama za vidole unalenga kuwazuia wahamiaji kutoweza omba tena hifadhi katika mataifa mengine lakini kwa mujibu wa ushuhuda uliotolewa na wahamiaji karibu 170 kumekuwa na unyanyasaji hata kwa watoto wadogo. Baadhi ya wahamiaji hawataki kuchukuliwa alama za vidole kwa matumaini ya kuendelea na safari katika mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya na kuomba hifadhi.

Kwa mwaka jana pekee Ulaya ilishuhudia wimbi kubwa la wakimbizi na waomba hifadhi zaidi ya milioni moja ambao wanakimbia vita na umaskini katika mgogoro mbaya kushuhudiwa tangu vita ya pili ya dunia.

Mhamiaji aliyewasili kisiwani Lampedusa akipatiwa msaada
Mhamiaji aliyewasili kisiwani Lampedusa akipatiwa msaadaPicha: AP

Mtafiti wa shirika hilo kwa Italia Matteo de Bellis amesema katika viongozi wa Umoja wa Ulaya wamezishinikiza mamlaka za Italia katika kiwango cha mwisho na zaidi katika jitihada za kupunguza harakati za wakimbizi kuingia katika mataifa mengine ya Ulaya. "Wahamiaji wengi wanakataa kuchukuliwa alama za vidole kwa sababu wanataka kwenda katika mataifa mengine ya Ulaya ambako wanadhani huenda wakakutana na ndugu zao. Lakini wanapokataa, maafisa wa Italia wanatumia nguvu dhidi yao. Na tumepokea ushuhuda wa watu ambao wametuambia kuwa wamepigwa, makofi na mateke na polisi wa Italia" amesema mtafiti huyo.

Mtafiti huyo anasema vitendo hivyo vinaleta hofu kwa wakimbizi ambao huwasili Italia badaa ya safari ndefu na ya tabu na wakati mwingine kunyanyaswa wakiwa mikononi mwa polisi na kufukuzwa kinyume na sheria.

Katika kesi 26 ambazo shirika hilo imezirekodi za unyanyasaji, 16 zinahusisha upigwaji na katika kesi karibu zote watu wamesema pia walipigwa na vifaa vya umeme akiwepo kijana wa miaka 16 akitokea Sudan. Kijana huyo anasema hivi na hapa namnukuu, "walinipiga na fimbo ya umeme mara nyingi katika mguu wangu wa kushoto na kisha kulia, kifuani na tumboni. Niliishiwa nguvu, sikuweza kupinga na katika hatua hiyo walichukua mikono yangu na kuifunga katika mshine" mwisho wa kunukuu.

Basi la Italia likiwa limewabeba baadhi ya wahamiaji mjini Rome
Basi la Italia likiwa limewabeba baadhi ya wahamiaji mjini RomePicha: picture-alliance/dpa/M. Percossi

Matteo anasema tena kamba "tunachoweza sema nimkwamba tumepokea kesi 24 za watu watu waliotuambia kuwa wametendwa vibaya. Katika mtazamo wetu, tunaona hii ni idadi kubwa na ni muhimu kwa mamlaka za Italia kutazama nini kinaendelea na kulitatua tatizo".

Utekelezaji wa mbinu hiyo unazifanya mamlaka za Italia kufanya mambo matatu katika kuwashughulikia wahamiaji, kwanza ni kuzichukua alama za vidole kwa watu wote wanaowasili katika bandari za Italia, kisha kuwatenganisha wakimbizi na wale wanaodhaniwa kuwa wahamiaji wa kawaida na mwisho ni mchakato wa kuwafukuza wahamiaji wa kawaida.

Mwandishi: Sylvia Mwehozi/AFP

Mhariri: Grace Patricia Kabogo