1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Zaidi ya 30 wauawa katika mashambulizi ya chekechea Thailand

6 Oktoba 2022

Zaidi ya watu 30, wengi wao wakiwa watoto, wameuawa Alhamisi wakati mwanaume mwenye silaha alipofyatua risasi katika shule ya chekechea kaskazini-mashariki mwa Thailand, maafisa wamesema.

https://p.dw.com/p/4HpVo
Thailand Massenerschießung in einer Kindertagesstätte
Picha: TPBS via REUTERS

Polisi imesema mashambuliaji huyo ambaye alikuwa na bunduki, bastola na kisu alifyatua risasi kwenye kituo cha kuangalia watoto katika mkoa wa Nong Bua Lam Phu majira ya saa sita na nusu mchana na kisha kukimbia eneo la tukio kwa kutumia gari.

Msemaji wa ofisi ya waziri mkuu wa Thailand, Anucha Burapachaisri, amethibitisha tukio hilo na kusema idadi ya vifo ni watu wasiopungua 30.

Kanali wa polisi Jakkapat Vijitraithaya kutoka mmkoa lilikofanyika shambulizi hilo, amemtambua muuaji kuwa ni Panya Khamrab, ambaye alikuwa luteni kanali wa polisi aliefukuzwa jeshini mwaka jana kwa kutumia madawa ya kulevya.

Thailand Massenerschießung in einer Kindertagesstätte
Mkuu wa polisi ya taifa ya Thailand, Damrongsak Kittiprapat, akizungumza na timu ya operesheni ya polisi mkoani Nong Bua Lam Phu, kufuatia mauaji ya watu wengi kwenye shule ya chekechea, Oktoba 6, 2022.Picha: Royal Thai Police/AFP

Kanali Kakkapat amesema mshukiwa huyo baada ya kufanya mauaji hayo alikwenda nyumbani kwake na kumuuwa mke wake na mtoto na kisha akajiuwa mwenyewe. Watoto waliouawa katika chekechekea ni wenye umri wa kati ya miaka mwili na mitatu.

Picha za vidio zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha shuka zikiwa zimefunika kile kilichoonekana kama miili ya watoto waliokuwa wamelala katika madimbwi ya damu katika shule iliyoko mji wa Uthai Sawan, umbali wa kilomita 500 kaskazini mashariki mwa Bangkok.

Soma pia: Muuwaji wa watu 20 auwawa

Mauaji hayo ya watu wengi yametokea chini ya mwezi mmoja baada ya afisa wa jeshi kuwapiga riasi na kuwauwa wenzake wawili kwenye kambi ya mafunzo ya kijeshi katika mji mkuu wa Bangkok.

Visa vya mauaji ya watu wengi vyaongezeka

Wakati Thailand ina idadi kubwa ya watu wanaomiliki bunduki, mauaji ya watu wengi ni nadra kutokea, lakini katika kipindi cha mwaka mmoja uliyopita, kumekuwa na alau visa vingine viwili vya mauaji ya bunduki yaliofanywa na wanajeshi walioko kazini, kulingana na gazeti la Bangkok Post.

Thailand Massenerschießung in einer Kindertagesstätte
Wafanyakazi wa afya wakitoa machela kwenye gari la wagonjwa katika mkoa wa kaskazini mwa Thailand wa Nong Bau Lam Phu, ambako askari wa zamani aliuwa watu wasioungua 30, wengi wao wakiwa watoto wa chekechea, Oktoba 6, 2022.Picha: Thai PBS/AFP

Mnamo mwake 2020, katika mmoja ya matukio mabaya zaidi ya mauaji katika taifa hilo la kifalme, mwanajeshi aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu 29 katika ghasia zilizodumu masaa 17 na kuwajeruhi wengine 57 kabla ya kupigwa risasi na makomando.

Soma pia:Ghasia za kisiasa zaitingisha Bangkok 

Mauaji hayo ya watu wengi, yaliohusishwa na mzozo wa deni kati ya muuaji, Sajenti-Meja Jakrapanth Thomma, na afisa mwandamizi, yalizusha hasira za umma dhidi ya jeshi.

Mwanajeshi huyo aliweza kuiba bunduki za mashambulizi kutoka ghala la jeshi kabla ya kuanza mauaji yake, huku akionesha matukio yake moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii.

Wakubwa katika jeshi walijaribu kumuonesha muuaji huyo kama mwanajeshi alieasi.

Chanzo: rtre, AP,