1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Thailand avuliwa madaraka kuelekea uamuzi

24 Agosti 2022

Mahakama ya Katiba ya Thailand leo imemsimamisha kazi Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha wakati ikifanya uamuzi wa ikiwa mtu huyo aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka wa 2014 alikiuka sheria ya ukomo wa muhula.

https://p.dw.com/p/4Fz2l
Thailand | Prayuth Chan-ocha
Picha: Sakchai Lalit/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo inafungua ukurasa mpya wa machafuko katikasiasa za nchi hiyo inayokumbwa na misukosuko. Kuondolewa kwa Chan-ocha kunatazamiwa kuwa tu kwa muda kwa sababu mahakama hiyo kwa jumla imekuwa ikitoa uamuzi wa kuipendelea serikali katika mfululizo wa kesi nyingine za kisiasa.

Uamuzi wowote wa kumruhusu jenerali huyo kubakia madarakani unachochea kuanzisha vuguvugu la maandamano ambalo kwa muda mrefu limetaka kumuondoa na kuanzisha mpasuko mkubwa nchini Thailand, nchi ambayo imekumbwa na vurugu za mara kwa mara za kisiasa tangu mapinduzi yaliyomuangusha aliyekuwa Waziri Mkuu Thaksin Shinawatra mnamo mwaka wa 2006.