1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO kukutana kukijadili kirusi cha Corona

11 Februari 2020

Shirika la afya ulimwenguni linatarajiwa kukutana kwa ajili ya kuangazia swala la ugonjwa wa virusi vya Corona huko China na ulimwenguni kote, huku idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo vikiendelea kupanda.

https://p.dw.com/p/3Xami
China Peking Besuch Präsident Xi Jinping
Picha: Reuters/Xinhua

Watu zaidi ya 1000 tayari wamekufa kutokana na ugonjwa wa Conora hali hiyo imelipa wasiwasi mkubwa shirika la afya ulimwenguni WHO ambalo lituma kikosi cha wataalamu wake nchini China.

Ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa CoronaVirus nje ya China limekuwa ni changamoto kubwa kuhusu kuenea kwa ugonjwa huo duniani.

Viongozi wa China wametangaza vifo vya watu 108 mnamo kipindi cha masaa 24 na kufikia hii leo waliofariki ni jumla ya watu 1,016 huko China bara , Hong Kong na Macao.

Lakini taarifa ya viongozi wa China inaelezea kwamba idadi ya visa vya walioambukizwa na ugonjwa huo imepungua toka wiki iliopita.

Jumatatu watu 2,478 walielezewa kuambukizwa ukilinganisha na siku iliopita ambapo walikuwa zaidi ya 2,500 huku idadi jumla ya walioambukizwa ikifikia 42,000.

Rais wa China Xi Jinping alitoa mwito mnamo Jumatatu wa kuchukuliwa ''hatua kubwa' kwa ajili ya kupambana maambukizi zaidi ya ugonjwa huo.

Visa kadhaa vya ugonjwa wa virusi vya Corona vinaripotiwa pia kwenye nchi zingine zikiwemo Ufilipino na Ufaransa.

Ni muhimu kuvidhibiti virusi vya Corona ndani na nje ya China

Tedros Adhanom Ghebreyesus -Generaldirektor der Weltgesundheitsorganisation (WHO)
Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: picture-alliance/S. Di Nolfi

Kiongozi wa  shirika la afya ulimwenguni, Tedros Adhanom Ghebreyesus amelezea kwamba umuhimu hivi sasa ni kutokuweko na visa zaidi ndani na nje ya china.

'' Kuweko kwa idadi hiyo japo kuwa ndogo ya watu waliona virusi vya Corona inaweza kuwa kibiriti kitakachosababisha moto mkubwa.Lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba ugonjwa huo umebaki katika maeneo yaliodhibitiwa hivi sasa''.

Tedros amesema kwamba hadi sasa visa vya watu walioambukizwa ugonjwa huo vilikuwa ni wale waliotokea kwenye jimbo la Wuhan, ulikoanzia ugonjwa huo.

Nje ya China bara ,watu wawili wamefariki kutokana na ugonjwa huo, mmoja Ufilipino na mwengine Hong Kong. Na visa vingine 400 kuripotiwa katika nchi zaidi ya thelathini.

Uingereza ilitangaza jumatatu kwamba ugonjwa huo ni tishio kubwa kwa afya ya umma nchini humo.

Huku ikiwaweka waliombukizwa virusi hivyo kwenye karantini. Mawaziri wa afya wa nchi za umoja wa ulaya watakuta kwenye kikakao cha dharura alhamisi mjini Brussels ilikutathmini na kuchukuwa hatua za pamoja katika kupambana na ujongwa huo.

Chanzo: AFP