1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mazingira wa Ujerumani aridhika na matokeo ya mkutano wa Postdam

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHr

Postdam:

Kwa mujibu wa waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigmar Gabriel, mawaziri wenzake wa kutoka mataifa manane tajiri kwa viwanda na wale wa mataifa matano yanayoinukia wamepiga hatua muhimu mbele katika juhudi zao za kusaka namna ya kuhifadhi hali ya hewa.Baada ya makutano wao mjini Postdam,karibu na mji mkuu wa Ujerumani ,Berlin,mawaziri wa mazingira wa mataifa tajiri kwa viwanda G8 na wenzao wa kutoka Jamhuri ya Umma wa China,India,Brazil,Mexico na Afrika kusini wamefikia maridhiano kuhusu mada kadhaa za mabishano.Makubaliano halisi lakini ya jinsi ya kuhifadhi hali ya hewa bado hayakupatikana.Waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigmar Gabriel amesema majadiliano thabiti yatafanyika mwezi June ujao wakati mkutano wa kilele wa viongozi wa G8 utakapoitishwa nchini Ujerumani na wakati mkutano wa kilele kuhusu hali ya hewa utakapoitishwa december ijayo nchini Indonesia