1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mazingira Irak anusurika kuuwawa.

23 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiV

Baghdad:

Waziri wa mazingira wa Irak bibi Narmine Othman amesema amenusurika katika jaribio la kutaka kumuuawa . Bibi Othman ambaye ni Mkudri alisema watu waliokua na silaha waliishambulia kwa risasi gari yake na kuwajeruhi walinzi wake watatu. Shambulio hilo lilitokea jana alipokua akielekea Baghdad baada ya likizo fupi katika jimbo la kaskazini la Kurdistan. Bibi Othman ni mwanachama wa chama cha Patriotic Union of Kurdistan-PUK cha Rais Jalal Talabani,