Waziri wa Italia Di Maio akutana na serikali mpya ya Libya
22 Machi 2021Matangazo
Waziri wa mambo ya nje Luigi Di Maio alikutana na Waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah mjini Tripoli ambapo walizungumzia uhusiano wa mataifa hayo mawili pamoja na masuala ya uhamiaji.
Dbeibah na Di Maio walijadili pia uwepo wa kamati ya pamoja itakayowawezesha kuzindua uhusiano wa kibiashara na maendeleo kati ya mataifa hayo mawili.
Di Maio amesema zaidi ya mwaka mmoja tangu kufanyika mkutano wa Berlin, sasa kuna Libya mpya iliyo na taasisi zilizoungana na zinazozawakilisha pande zote.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Italia pia alikutana na kiongozi wa Baraza la uais nchini Libya Mohammad Younes Menfi, pamoja na manaibu wake wawili.