JamiiAsia
Waziri Mkuu wa zamani wa China Li Keqiang amefariki dunia
27 Oktoba 2023Matangazo
Taarifa ya shirika la habari la nchini humo limesema Keqiang amekutwa na umauti baada ya kupatwa ghafla na shambulio la moyo.
Kulingana na taaarifa hiyo, waziri mkuu huyo wa zamani alianzakuugua Alhamisi na alikufa baada ya juhudi za kuokoa maisha yake kugonga mwamba.
Li Keqiang alijiuzulu wadhifa wake Machi 10 baada ya kuwa miaka 10 madarakani chini ya utawala wa Rais Xi Jinping. Kwa miaka mingi kumekuwa na uvumi kuhusu afya ya Keqiang.
Baadhi ya wanadiplomasia waliwahi kusema katika mazungumzo ya faragha kuwa, wakati wa ziara zake nje ya China ratiba za Li Keqiang zilitawaliwa na vipindi virefu vya mapumziko.