Raimondo na Le Keqiang watoa wito wa ushirikiano
29 Agosti 2023Matangazo
Ziara ya waziri Raimondo nchini China inafuatia nyingine za hivi karibuni zilizofanywa na wajumbe wa Marekani wa ngazi za juu kwa lengo la kupunguza mivutano na China, nchi inayoshika nafasi ya pili duniani katika nguvu za kiuchumi.
Waziri wa biashara wa Marekani amemwambia waziri mkuu wa China kwamba, Marekani inataka kushirikiana na China katika masuala muhimu ya dunia, ikiwa pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, teknolojia ya akili bandia na katika juhudi za kupambana na uraibu wa madawa makali yanayotumika kutuliza maumivu.
Waziri huyo wa Marekani pia leo hii alikutana na viongozi wengine wa China ambapo alisisitiza umuhimu wa kuweka wazi njia za mawasiliano baina ya mataifa yao makubwa.