1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa zamani DRC aachana na azma ya kuwania urais

20 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Augustin Matata Ponyo ameachana na azma yake ya kuwania urais na badala yake, ameeleza kumuunga mkono mgombea atakayeteuliwa na muungano wa upinzani.

https://p.dw.com/p/4Z9o7
Waziri Mkuu wa zamani wa DRC Augustin Matata Ponyo
Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Augustin Matata PonyoPicha: Florida Zantoto/Press Office Primeminister Kongo

Hii ni kufuatia mapendekezo ya wagombea wanne wa upinzani waliokutana Afrika Kusini wiki iliyopita.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Waziri Mkuu huyo wa zamani amesema atamuunga mkono Moise Katumbi, mfanyibiashara tajiri na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga.

Katumbi anatarajiwa kuzindua kampeni yake leo Jumatatu.

Wawakilishi wa vyama vikuu vya upinzani nchini Kongo walifanya mazungumzo mjini Pretoria wiki iliyopita kuhusu jinsi ya kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu wa Disemba 20 utafanyika kwa njia huru na ya haki na kuamua juu ya mgombea mmoja atakayemenyana na Rais Felix Tshisekedi.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaanza kampeni ya uchaguzi ya mwezi mmoja kuanzia leo Jumatatu huku tayari wagombea 26 wakionyesha nia ya kuwania urais.