1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Uturuki kutembelea Somalia

18 Agosti 2011

Waziri Mkuu wa Uturuki, Tayyip Erdogan leo anatarajiwa kwenda nchini Somalia akiwa na familia yake kutembelea kambi za misaada ya kiutu ambapo anafuatana pia na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo, Ahmet Davutoglu.

https://p.dw.com/p/12ImK
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: AP

Erdogan amesema Uturuki inategemea kufungua hospitali sita nchini humo, kutuma tani 20 za madawa na tani 10 ya vyakula.

Nae Waziri wa kwanza kufika katika eneo hilo la vita kwa zaidi ya miaka 18, Andrew Mitchell wa anaeshughulikia maendelea ya kimataifa wa Uingereza amehimiza hatua za haraka kuwanusuru raia wa Somalia

Amesema kiasi cha watoto 400,000 wako hatarini kupoteza maisha ambapo pia alitangaza msaada wa kiasi cha euro milioni 29. Amesema pasipo hatua za haraka basi dunia itashuhudia maafa kama yale yalitokea 1991 na 92.

Somalia Dürre Hungersnot Flüchtlingslager in Mogadischu Mann mit totem Kind
Kambi ya misaada ya kiutuPicha: dapd

Waziri Mitchell alitembelea kambi kadhaa za misada ya kiutu ambazo zinawatunza watu waliokimbia njaa.

Mwenyekiti wa Shirika la Misaada ya Chakula la Ujerumani, Bärbel Dieckman aliwasili mjini Mogadishu hivi karibuni na hapa anaelezea laichokishuhudia.

"Nilichoshuhudia kinasikitisha, ni kwa nadra, nimeona mtu anakuwa hana la kufanya juu ya shida zinazomkabili, nazungumzia watu laki 4 waliokuwemo kwenye kambi hiyo. Wanahudumiwa lakini hawana matumaini"

Awali katika mkuztano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC) uliofanyika mjini Instanbul, nchi wanachama ziliahidi kuchangia kiasi cha dola milioni 350 kama msaada wenye lengo la kukabiliana na baa la njaa nchini Somalia.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Jenerali Ekmeleddin Ihsanoglu, amesema kiasi ya Wasomali milioni 3.7 wako katika hatari kubwa kutokana na uhaba wa chakula na kuongeza kuwa anatarajia kwamba mchango huo wa fedha utafikia dola milioni 500.

Aidha amezitaka nchi hisani kusadia katika mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na ukame nchini Somalia na hasa katika katika ujenzi wa miundombinu na ustawi wa kilimo.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo uliyoudhuriwa na mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa 57 yaliyo wanachama wa OIC, Waziri Mkuu Erdogan alisema janga la Somalia ni jaribio lingine la utu sio tu kwa Waislam bali kwa watu wote.

Waziri Mkuu huyo aliwakumbusha matajiri na hasa katika nchi za magharibi kujitoa katika kusadia umma wa watu katika eneo la Pembe ya Afrika.

Wakati huo huo Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaandaa mkutano ambao pamoja na mambo mengine utajadili namna ya kuweza kusaidia Somalia.

Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Addis ababa nchini Ethiopia, unafanyika wakati FAO imekwishatangaza kuwepo kwa tatizo la ongezeko la bei ya chakula duniani.

Watu milioni 12 kutoka katika maeneo ya Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia na Uganda wanakabiliwa na baa la njaa lililotokana na ukame mbaya zaidi kutokea kwa miongo kadhaa.

Mwandishi: Sudi Mnette/DPA/AFP
Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed