1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Lebanon ajiuzulu

29 Oktoba 2019

Waziri mkuu wa Lebanon Saad al Hariri ametangaza kujiuzulu pamoja na serikali yake. Hariri amesema amegonga mwamba na kufikia ukingoni na hivyo atawasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa rais wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/3S9Pi
Libanon PK Premierminister Saad al-Hariri in Beirut
Picha: picture-alliance/dpa

Wimbi la maandamano limeikumba Lebanon kwa wiki mbili kudai serikali ijiuzulu kufuatia kuongezeka kwa ghadhabu dhidi ya viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na rushwa.

Wafuasi wa kundi la kishia la Hezbollah na Amal wamepambana na waandamanaji katika eneo la barabara lililowekwa vizuizi mjini Beirut na kuyaangusha mahema yao na kuwafanya polisi kuingilia kati.

Tukio hilo limeshuhudiwa baada ya watu kadhaa kulazimisha kuingia kwa mabavu kwenye kambi ya waandamanaji mjini Beirut kujaribu kufungua barabara iliyowekwa vizuizi.