1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wafariki kwa Ebola DRC

22 Februari 2021

Watu wanne wamekufa kutokana na maradhi ya Ebola baada ya mripuko mpya wa maradhi hayo kuanza mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku watu wakikaidi kuchukuwa hatua za kuudhibiti ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/3phDk
Kongo Mbandaka Ebola
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Bompengo

Kwa mujibu wa waziri wa afya wa jimbo la Kivu Kaskazini, Dk. Eugene Syalita, hadi sasa watu sita wamesajiliwa kuambukizwa Ebola na wamepoteza wanne kati yao. 

Waziri huyo wa afya amelalamikia tabia ya wakaazi wa Kivu Kaskazini kutokuuchukulia ugonjwa huo kwa umakini.

Mripuko huo ulipotokea miaka iliyopita, sehemu kubwa ya raia ilikuwa ikikanusha kuwepo kwake na kukataa kabisa kuchukuwa hatua za kuzuwia maambukizo, kama vile kugusana na kuziosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola. 

Wimbi la kumi la Ebola lililitangazwa tarehe 1 Agosti 2018 na kutokomozwa tarehe Juni 25 mwaka jana, likiwa limeangamiza watu 2,200, kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO.