1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 3,661 wameuawa 2024 katika ghasia za Haiti

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 3,600 wameuawa mwaka huu katika ghasia zinazofanywa na magenge ya uhalifu nchini Haiti.

https://p.dw.com/p/4lBs7
Matairi yakiwa yamechomwa moto Port-au-Prince, Haiti
Matairi yakiwa yamechomwa moto Port-au-Prince, HaitiPicha: Richard Pierrin/AFP

Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema takriban watu wegine  600,000 waliyakimbia makazi yao katika miezi sita ya kwanza ya 2024.

Ripoti hiyo iliyotelewa mjini Geneva imesema takriban watu 893, wakiwemo watoto 25, walitekwa nyara na kushikiliwa na makundi ya wahalifu, ambayo yanawania madaraka katika ombwe lililoachwa wazi na mgogoro wa kisiasa na mamlaka dhaifu ya serikali.

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema maisha zaidi hayapaswi kupotea kwa uhalifu huo usio na maana. Huku akihimiza mamlaka ya Haiti na jumuiya ya kimataifa kufanya zaidi kuwalinda watu katika kisiwa hicho cha Caribbean.

Oktoba 2023, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kupeleka kikosi cha kimataifa cha kuleta utulivu. Kikosi hicho kinaongozwa na Kenya ambayo imepeleka polisi waatao 2,500 kusaidia polisi wa Haiti.