SiasaHaiti
Umoja wa Mataifa waonya kitisho kikubwa nchini Haiti
28 Septemba 2023Matangazo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwenye ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumatano kwamba machafuko yanayofanywa na magenge ya uhalifu yanazidi kuongezeka, na magenge hayo yanazidi kuimarisha udhibiti hadi nje ya mji mkuu Port-au-Prince.
Amesema uhalifu unaofanywa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia unaohusisha ubakaji wa makundi, na ambao umeendelea kutumiwa na wahalifu kuwatisha raia walio chini ya udhibiti wao.
Ripoti hiyo inatolewa wakati wanachama wa Baraza la Usalama la umoja huo wakijadiliana juu ya ujumbe wa usalama wa kimataifa, ulioombwa na mamlaka za Haiti ili kulisaidia jeshi lake la polisi lenye watumishi wachache na uhaba wa rasilimali.