Wanasiasa Pakistan waombwa kuwa wakomavu wa kisiasa
10 Februari 2024Hatua hiyo imepelekea chama kinachopendelewa na jeshi kuanza harakati za kuunda serikali ya pamoja ili kuongoza.
Katika siku za hivi karibuni, taifa hilo la Kusini mwa Asia limeshuhudia ushindani mkali wa kisiasa, baada ya wagombea huru na watiifu kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyefungwa jela Imran Khan kukizuia chama kinachoungwa mkono na jeshi cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) kupata wingi wa kura.
Pakistan yapongezwa kwa zoezi zuri la uchaguzi
Chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kilikabiliana na ukandamizaji dhidi yake na uliodumu kwa miezi kadhaa, ambao ulififisha kasi ya kampeni na kuwateua wagombea huru ambao wameleta ushindani mkubwa kwa wapinzani wao.
Jeshi limewahi kuhanikiza katika siasa za Pakistan, ambapo majenerali wake wamekuwa wakiiongoza nchi hiyo takriban nusu ya historia yake tangu ilipojitenga na India mnamo mwaka 1947.