1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Gaddafi wawarudisha nyuma waasi

Halima Nyanza9 Machi 2011

Wanajeshi watiifu kwa Kanali Muammar Gaddafi wa Libya wanaripotiwa kufanya mashambulizi makali dhidi ya waasi wa nchi hiyo kwa kutumia mizinga, maroketi na ndege za kivita.

https://p.dw.com/p/10Vf9
Vikosi vitiifu kwa Gaddafi vinawarudisha nyuma waasi
Vikosi vitiifu kwa Gaddafi vinawarudisha nyuma waasiPicha: AP

Huku jeshi la Gaddafi likijizatiti kwa mashambulizi zaidi, madhara ya mapigano haya, vikiwemo vifo majeruhi na tishio la wimbi la wakimbizi, yamekuwa yakiongeza shinikizo kwa serikali za kigeni kuchukua hatua, ingawa wengi wanahofia matokeo ya uingiliaji kati kijeshi.

Uingereza na Ufaransa zinalichagiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuzuia ndege kutoruka juu ya anga ya Libya, hatua ambayo italizuia jeshi la Gaddafi kufanya mashambulizi ya anga.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, amesema uamuzi huo wa kuzuia ndege kuruka, unatakiwa uidhinishwe na usimamiwe wa na Umoja wa Mataifa na siyo juhudi zitakazoongozwa na nchi yake tu.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya unapanga kuiwekea Libya vikwazo vipya.