1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOM lahofia vifo vya baharini kuchukuliwa kawaida

2 Oktoba 2023

Mkuu mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uhamiaji IOM Amy Pope ameelezea wasiwasi wake kwamba vifo vya wahamiaji na wakimbizi katika bahari ya Mediterenia vimekuwa vikichukuliwa kama kitu cha kawaida.

https://p.dw.com/p/4X3OG
Wahamiaji 61 waliokuwa wakisafiri katika boti ya mbao waliokolewa na meli ya uokozi ya Geo Barents inayoendeshwa na Madaktari wasio na Mipaka, MSF, Septemba 28, 2023
Wahamiaji 61 waliokuwa wakisafiri katika boti ya mbao waliokolewa na meli ya uokozi ya Geo Barents inayoendeshwa na Madaktari wasio na Mipaka, MSF, Septemba 28, 2023Picha: DARRIN ZAMMIT LUPI/REUTERS

Bi Amy Pope ameapa kufanya kazi na serikali husika kutoa njia mbadala za kiuchumi kushughulikia mgogoro uliopo wa wahamiaji.

Pope ambaye ni mshauri wa zamani wa Ikulu ya Marekani ameanza majukumu yake katika shirika hilo la IOM hii leo wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa juu ya wahamiaji.

Amy Pope amesema ziara yake ya kwanza itakuwa katika mataifa ya Afrika Mashariki atakakokutana na wajumbe wa kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia kisha ataelekea mjini Brussels kukutana pia na maafisa wakuu wa Ulaya kujadili na kutafuta mpango wa kushughulikia uhamiaji usio wa kawaida.