Wafanyakazi wa shrika la ndege la Afrika Kusini wagoma
15 Novemba 2019Matangazo
Shirika hilo halijatengeza faida tangu mwaka 2011 na halina kiongozi mkuu wa kudumu limesema mgomo huo wa vyama vya wafanyakazi unaohusisha wafanyakazi 3000 kati ya 5000 waliopo unasababisha hasra ya hadi dola milioni 3.4 kwa siku na unatishia hatma yake.
Vyama vya wafanyakazi vimekataa pendekezo la nyongeza ya mshahara lililotolewa jana na pia wanagomea mipango ya shirika hilo la ndege ya kutaka kupunguza wafanyakazi zaidi ya 900 ili kukabiliana na hali mbaya ya kifedha na kuepuka mipango ya uokozi kutoka serikalini.
Kaimu mkuu wa masuala ya fedha wa SAA amekiambia kituo kimoja cha habari kuwa shirika hilo limeathiriwa na utendaji wa wasimamizi waliotangulia na linapaswa kufanyiwa mageuzi.