Wachungaji wanaotuhumiwa na mauaji kufikishwa mahakamani
2 Mei 2023Paul Nthenge Mackenzie aliyejitangaza kuwa mchungaji na kuunda kanisa lake linaloitwa Good News International mwaka 2003 anatuhumiwa kuwachochea wafuasi wake kuishi bila ya kula wala kunywa chochote mpaka wafe na kukutana na Yesu, alifikishwa mahakama ya Malindi kujibu kesi.
Jamaa na familia za wahanga walimiminika ndani ya chumba kidogo cha mahakama hiyo, Mackenzie akisindikizwa na maafisa kadhaa wa polisi akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanane.
Waendesha mashtaka mjini Mombasa wanataka Mchungaji mwingine maarufu Ezekiel Odero ambaye ana utajiri mkubwa nchini humo azuiliwe kwa siku nyingine 30 zaidi.
Mchungaji huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Mombasa, baada ya kukamatwa alhamisi wiki iliyopita, akituhumiwa kuhusika miongoni mwa mengine, kusaidia mauaji, utekaji nyara, kuchochea itikadi kali za kidinina uhalifu dhidi ya ubinadamu.