1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaanza upasuaji wa miili ya waliofukuliwa Shakahola

1 Mei 2023

Maafisa nchini Kenya wanasema shughuli ya upasuaji wa zaidi ya miili 100 inayohusishwa na mchungaji mmoja ambaye anadaiwa kuwashauri waumini wake wafunge kula hadi wafe ili wawe wa kwanza kwenda mbinguni, umeanza.

https://p.dw.com/p/4Qkt5
Todesfälle durch Kulte in Kenia
Picha: Stringer/AA/picture alliance

Mpasuaji mkuu wa serikali ya Kenya, Johansen Oduor, ndiye anayeongoza shughuli hiyo ya upasuaji. Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Kithure Kindiki, amesema upasuaji huo utachunguza kila chanzo cha vifo hivyo na iwapo baadhi ya miili ilikuwa haina viungo.

Uchunguzi wa maiti za maafa ya msitu wa Shakahola waanza

Wafuasi 109 wa kanisa la Good News International Church lililo na makao yake katika msitu wa Shakahola katika eneo la Malindi katika pwani ya Kenya, wanaaminika kufariki dunia kufikia sasa.

Mchungaji wa kanisa hilo, Paul Mckenzie, anazuiliwa na polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho.