1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi habari watatu wauguza majeraha ya risasi za mpira

31 Oktoba 2019

Wandishi habari nchini Uganda wametangaza kususia vikao vya habari vya polisi kupinga kile wanachokitaja mwenendo wa kuwashambulia wakiwa kazini.

https://p.dw.com/p/3SFzQ
Uganda Medienfreiheit Proteste 20.05.2013
Picha: Reuters

Picha zinazoonesha majeraha makubwa waliopata wandishi habari watatu wakati walipokuwa wakifuatilia makabiliano kati ya polisi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere zimeibua hasira miongoni mwa wandishi habari.

Wandishi hao wana vidonda na michubuko ambayo madaktari wamelezea kuwa itahitaji matibabu ya hali ya juu ikiwemo upasuaji.

Huku wandishi habari hao wakiwa wamelazwa hospitalini, wenzao wameamua kususia vikao vya polisi vinavyoitishwa kila mara kwenye makao makuu ya jeshi hilo pamoja na vituo vingine vya polisi. Rais wa chama cha wanahabari UJA Bashir Kazibwe amesema…

Kwa upande wao polisi wamekanusha madai kuwa askari wake walikusudia kuwashammbulia wanahabari. Wamewalaumu wanahabari kwa kutojiweka maeneo salama wakati wa makabiliano na wanafunzi.

Polisi walaumiwa kuwazuwia waandishi habari kutekeleza kazi zao

Uganda «Präsident der Ghettos» Bobi Wine wegen Hochverrats angeklagt
Polisi mjini Kampala wakishika doriaPicha: picture-alliance/AP Photo/R. Kabuubi

Lakini wandishi habari waliojeruhiwa wanasisitiza kuwa jinsi walivyoshambuliwa ni wazi kwamba polisi hawakutaka watekeleze kazi zao katika mazingira hayo ili kuonyesha hali halisi ya mambo. Kwa mfano bomu moja la kutoa machozi lilimlipukia mmoja wao mapajani. Wabunge wameshutumu vitendo hivyo kwa kusema..

Katika kipindi cha wiki mbili ambapo ghasia za wanafunzi zimedumu, wandishi habari walinyanyaswa kwa namna mbalimbali. Baadhi walikamatwa na kulazimishwa kufuta picha na video walizorekodi.

Vitendo hivyo ndivyo wanahabari wanaelezea kuwa ni hila za polisi kuwakosesha kufanya kazi yao ya kupasha jamii habari kuhusu uhalisi wa mambo. Huku mgongo wa wandishi habari dhidi ya polisi ukianza kufanyika leo, watu katika taaluma hiyo wamehimizwa kutowasaliti wenzao kwa kuitikia na kuhudhuria shughuli na vikao vya polisi.

Aidha, wandishi habari watafanya maandamano ya amani wiki ijayo wakielekea bungeni watakakowasilisha malalamiko yao kwa spika wa bunge. Aidha watawasilisha malalamiko kwa mkuu wa jeshi la polisi. Bashir Kazibwe amesema….

Angalau hali ni tulivu katika chuo kikuu cha Makerere lakini polisi wamendelea kuweka doria na hakuna mwanahabari anaruhusiwa kuingia chuoni hapo.

Emmanuel Lubega DW Kampala