MigogoroSudan
Vita na uporaji vyaripotiwa katikati mwa Sudan
1 Julai 2024Matangazo
Kwa mujibu wa makundi ya haki za binadamu na wakaazi walioshuhudia, uvamizi huo umewalazimu maelfu ya watu kukimbia.
Wanamgambo wa RSF waliokuwa ndani ya magari ya wazi wakiwa na bunduki walivamia mji wa Singa ulio kilometa 350 kusini mashariki mwa mji mkuu Khartoum.
Soma pia: UN: Sudan yakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula
Mapambano hayo yaliyoanzishwa na RSF mapema wiki hii yalianza kwa kundi hilo kushambulia kijiji cha Jebal Moya kabla ya kuendelea katika eneo la Singa.
Mapema Jumamosi RSF ilidai kuteka jengo kuu la jeshi huko Singa.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Sudan Brigedia Nabil Abdalla amesema kuwa jeshi lilifanikiwa kukomboa eneo hilo na kuwa mapigano yaliendelea hadi Jumapili asubuhi.